Kamishna wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa amemuagiza Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko kuwavua madaraka Wakuu Watatu (3) wa vituo vya Elimu ya Watu Wazima kutokana na kukiuka utaratibu wa kuchagua wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza kuwaingiza katika Mfumo wa Elimu ya Watu Wazima.
Profesa Eustella ameyasema hayo leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam .
Amesema
kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakishirikiana na Halmashauri baada ya
kuchagua wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wamefanya vizuri wao
huchukua wanafunzi waliofeli na kuwapeleka katika shule za serikali
wakidai kuwa wanafunzi wamechaguliwa katika chaguo la pili.
Baada
ya kuchaguliwa wanafunzi hao wakifika shule wanadaiwa ada wakati
serikali imesema elimu ni bure, hali inayowachanganya wazazi.
Wakuu wa vituo waliovuliwa madaraka ni Wotugu Mganda (Dar es Salaam), Senorina Kateule (Dodoma),Steward Ndandu Geita na (Mwanza).
Profesa
Eustella amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakidandia matokeo ya
kidato cha kwanza kwa kufanya upotoshaji kwa wazazi wakati wanafunzi
wanaosoma katika elimu ya watu wazima ni hiari kutokana na sera ya
elimu.
Wanafunzi
ambao wamechaguliwa kwa mwaka huu wamekuwa wakidai ada ya sh. 80,000
hadi 250,000 na ndipo malalamiko yakaanza kwa wazazi baada ya kudaiwa
ada hiyo.
Profesa
Eustella, amesema kuwa mmoja wanafunzi katika Mkoa wa Dar es Salaam
aliambiwa amefaulu katika chaguo la pili katika shule ya sekondari ya
Oasterbay .Baada ya kufika shuleni, mwanafunzi huyo alikuta mambo
tofauti kwa kudaiwa ada na kuambiwa awasiliane na Taasisi ya Elimu ya
Watu Wazima.
0 comments:
Post a Comment