Mawakili kiongozi wa upinzani nchini
Uganda Kizza Besigye wamesema watawasilisha kesi mahakamni leo
kulalamikia kuendelea kuzuiliwa kwake an polisi.
Alikamatwa
alipokuwa katika makao makuu ya chama chake cha FDC Ijumaa, siku moja
kabla ya kutangazwa kwa matokeo, na akarejeshwa kwake nyumbani baadaye
jioni.
Amekuwa akikamatwa kila anapojaribu kuondoka nyumbani kwake na kisha kurejeshwa baadaye jioni.
Polisi wamekuwa wakizingira nyumba yake na kuwazuia watu kuingia. Chama hicho kimepinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Jumamosi ambapo Rais Museveni alitangazwa mshindi.
Mawakili wake pia wanatafakari uwezekano wa kuwasilisha kesi kortini kupinga matokeo hayo ya urais.
Bw Besigye amelalamika vikali kutokana na hatua ya kuzuiliwa nyumbani na maafisa wa usalama.
Ujumbe uliopakiwa kwenye ukurasa wake wa Facebook, baada yake
kurejeshwa nyumbani kwake Alhamisi, unasema: “Jioni hii, najihisi kama
naweza kuwa ‘gaidi’ halisi.”
Amesema iwapo kuna sababu ya
kumzuilia, basi anafaa kuzuiliwa gerezani au eneo lililotangazwa kuwa
seli la sivyo aachiliwe huru na kuruhusiwa kutembea.
Alhamisi
alikamatwa alipokuwa akijaribu kuelekea afisi za FDC eneo la
Najjanankumbi mwendo wa saa tano mchana na akaachiliwa huru saa tatu
usiku.
Chanzao: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment