Adverts

Thursday, February 18, 2016

Read More Waziri Mbarawa Awakamua MAJIPU Wakurugenzi TCRA na TEMESA Kwa Utendaji Wao Usioridhisha

 
Waziri wa Ujenzi wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa ameagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, kusitisha mara moja mkataba wa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa mamlaka hiyo, Elizabeth Nzagi, kwa kushindwa kusimamia ufungwaji wa kifaa cha kufuatilia mapato ya simu ya ndani katika mitambo ya kuchunguza mapato katika mitandao ya simu (TTMS).

Waziri Mbarawa amesema kutokufungwa kwa kifaa hicho kumeisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 400/= hivyo ameiagiza pia bodi hiyo ya TCRA kuwasimamisha kazi mara moja, Kaimu Mkurugenzi anayesimamia mfumo wa uhakiki na usimamiaji huduma za mawasiliano, mhandisi Sunday Richard na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Modestus Ndunguru ili kupisha uchugnuzi dhidi ya uhusika wao katika kusababisha kifaa hicho kutokufungwa.

Aidha, Waziri Mbarawa ametoa onyo kali kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRCA, Ally Simba kwa kutokuwa makini katika utendaji huo huku akimwagiza kuhakikisha kuwa kifaa hicho kinafungwa ndani ya siku saba. 
Profesa  Mbarawa  pia  ametengua  uteuzi  wa  Mtendaji  mkuu  wa  Wakala  wa  Umeme  na  Ufundi  Tanzania  (Temesa),Mhandisi  Marcellin Magesa  kwa  kushindwa  kusimamia  matengenezo  ya  magari  ya  serikali, mitambo  na  vivuko.
Kadhalika, ametengua  uteuzi  wa  Mkurugenzi  wa  matengenezo  ya  magari  ya  serikali,Prisca  Mukama  na  Meneja  wa  Karakana   ya   magari  ya  Serikali  John Mushina  ambao  watapangiwa  majukumu mengine.

0 comments:

Post a Comment