Mh mkuu wa wilaya ya kinondoni leo ametangaza kuwa kuanzia sasa
walimu wote mkoa wa DAR watakuwa wanapanda kwenye daladala kwenda kazini
bure asubuhi na jioni saa tisa mpaka saa kumi na moja wakati wa
kurudi.Hii ni baada ya mh makonda kukubaliana leo na wamiliki wa
daladala, Na walimu wote watapewa vitambulisho maalumu.
Huyu ndio kiongozi tunayemtaka anayetenda mambo kwa vitendo na anayejali kero za wananchi wake ikiwemo walimu, sasa kwa mwanzo huu mzuri heshima ya walimu itarudi na ualimu utakuwa mzuri na kufanya walimu waongeze weredi katika ufundishaji.
Kipekee ninakupongeza sana mh mkuu wa wilaya makonda , najua wapo
wajinga wachache watakaokosoa kwa faida zao binafsi ambao kazi yao ni
kuropoka tu bt endelea kupiga kazi tunakukubali sana na tubakuombea
Mungu akulinde na ikimpendeza Rais akuteuwe uwe mkuu wa mkoa wa Dar.
0 comments:
Post a Comment