Waziri wa Kilimo na Mifugo Mwigulu Nchemba amefanya ziara ya Kushtukiza saa saba usiku wa kuamikia leo katika Machinjio ya Ukonga Mazizi.
Katika ziara hiyo, Waziri Nchemba amekamata ng'ombe
200 wakiwa wanaingizwa kwenye machinjio bila kibali halali, na kati yao ni ng'ombe
20 tu ndo walikuwa na kibali cha kuchinjwa, hivyo ushuru wa ng'ombe 180 ulikuwa unatafunwa na watumishi waovu.
Baada ya kubaini hali hiyo,Waziri Nchemba ameufukuza uongozi wote wa machinjio hayo na kuagiza vyombo vya dola viwakamate viongozi wote waliohusika na kuwafikisha mahakamani.
Adverts
Thursday, February 11, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment