Albamu mpya ya mwanamuziki Kanye
West imepakuliwa kutoka mtandaoni zaidi ya mara 500,000 kulingana na
kampuni ya kupakua kanda za video na sauti Torrent Freak.
Maelfu ya raia waliolipa ili kusikiza albamu hiyo walilalama kwamba wameshindwa kupakua albamu hiyo licha ya kuilipia.
Kwa sasa inaongoza miongoni mwa albamu zinazopakuliwa mitandaoni kwa njia ya wizi.
Albamu
hiyo imeonekana mara mbili katika mtandao wa usambazaji wa miziki kumi
bora iliopakuliwa,licha ya Kanye West kutuma ujumbe katika tweeter
akisema kuwa albamu hiyo itapatikana katika Tidal pekee.
Source: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment