TUNDU
Lissu, Mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pia
Mbunge wa Singida Magharibi leo jijini Dar es Salaam amehojiwa na Jeshi
la Polisi kuhusu hoja alizozitoa kwenye Gazeti la MAWIO.
Lissu
amehojiwa kwa zaidi ya saa moja Makao Makuu ya Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam baada ya kuhitajika kutoa maelezo kwa madai ya kutoa kauli
za uchoelezwa zilizoandikwa kwenye Gazeti la MAWIO zilizohusu mgogoro
wa kisiasa visiwani Zanzibar.
Habari
iliyoandikwa na gazeti hilo iliyobeba kichwa cha habari ‘Machafuko yaja
Zanzibar’ inaelezwa kuwa sababu ya serikali kulifungia gazeti hilo
tarehe 15 Januari mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kumaliza kutoa maelezo Lissu amesema,
serikali inajaribu kumziba mdomo asizungumzie kuhusu suluhu ya mgogoro
wa kisiasa unaoendelea visiwani Zanzibar wakati wahusika hawazingatii
misingi ya demokrasia.
“Wale
waliobebwa kwenye uchaguzi leo wanataka kutufumba midomo tusizungumzie
masula ya uchaguzi wa Zanzibar kwani machafuko yanaweza kutokea visiwani
humo kwa tahadhari hiyo wanatuita wachochezi,” amesema Lissu.
Amesema
kuwa, wao wametoa tahadhari ili yasitokee machafuko na umwagikaji wa
damu na kwamba, Rais John Magufuli atawajibika kwenye Mahakama ya
Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kama alivyowajibishwa Rais Uhuru
Kenyatta wa Kenya.
Amesema,
mahojiano yake na Gazeti la Mawio ndio yaliyosababisha yeye kuitwa na
kuhojiwa na polisi na kwamba, mtazamo wake ulioandikwa kwenye gazeti
hilo ndio umechangia kufutwa kwa gazeti hilo.
Amesema kuwa hatokubali kuzibwa mdomo hata kama watatumia nguvu ya polisi.
Amesema,
hatua ya Rais Magufuli kukakataa kujihusisha na mgogoro wa Zanzibar
haikubaliki kwa kuwa ndiye ndiye atakayepeleka jeshi pale vurugu
zitakapotokea.
Lissu amefika polisi hapo akiwa na mawakili wa watatu wa Chadema ambao ni Peter Kibatala, Fedrick Kiwelo na Hekima Mwasibu.
Amesema, baada ya mahojiano hayo polisi watapeleka jalada lake kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa hatua zaidi.
0 comments:
Post a Comment