Rais Barrack Obama amesaini vikwazo
zaidi dhidi ya Korea Kaskazini kuhusiana na mpango wake wa Nuklia, wiki
chache tu baada taifa hilo kufanya majaribio ya zana zake za mafasa
marefu.
Taifa hilo limekataa kusitisha mpango wake wa nuklia na mswada ulioidhinishwa na bunge la Congress wiki iliyopita.
Vikwazo hivyo vinajaribu kuzuia fedha ambazo Korea Kaskazini ilihitaji ili kuunda zana zaidi za nuklia.
Marekani na Uchina zinashauriana kuhusu azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na vikwazo hivyo vipya.
Uchina imesema kuwa baada ya mikakati hiyo huenda ikasambaratisha uchumi wa Korea Kaskazini.
Vikwazo
hivyo ni pamoja na kupiga tanji mali ya mtu yeyote anayefanya biashara
inayohusiana na mpango huo wa nuklia na silaha kwa Korea Kaskazini, au
kuhusika na ukiukwaji wa haki za kibinadam.
Mswada huo pia unaruhusu misaada ya dola milioni hamsini kusaidia
utoaji wa misaada ya kibinadamu na kupeperusha matangazo ya Radio nchini
Korea Kaskazini.
Hivi majuzi Korea Kaskazini ilifanya majaribio
ya zana zake za masafa marefu, kitendo ambacho wakosoaji wanasema
lilikuwa jaribio la kiteknolojia la zana za masafa marefu
Runinga
ya taifa nchini humo ilitangaza kuwa Korea Kaskazini ilikuwa imefanikiwa
kutuma mtambo wake wa Satelite katika anga za juu zaidi.
Source: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment