Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amewafuta kazi takriban watu ishirini
na sita ambao ni wakuu wa idara mbali mbali za serikali ikiwemo vyombo
vya habari.Maafisa hao wametakiwa kukabidhi madaraka kwa maafisa wa
ngazi za juu katika idara zao mpaka kutakapofanywa uteuzi mwengine.
Huu ni mwanzo wa mabadiliko makubwa ambayo yanatarajiwa kuathiri zaidi ya mamia ya idara za serikali.
Rais Buhari amepata shinikizo kubwa la kufanya mabadiliko hayo ambayo
yangewaachisha kazi maafisa wengi ambao walikuwa karibu na aliyekuwa
rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan. Nafasi zao zinatakiwa zichukuliwe
na wafuasi kutoka chama cha APC, hasa wale waliokuwa na mchango mkubwa
katika uchaguzi uliomwingiza madarakani rais Buhari.
Uteuzi wa nafasi hizo unaonekana kama ni bakshish kwa wale waliotumia
nguvu zao kukiingiza chama madarakani.Inasemekana, wale waliopewa nafasi
hizo mwanzoni, walizitumia kwa manufaa yao binafsi.
Lakini kutokana na ari aliyokuwa nayo rais Buhari ya kupambana na ufisadi, maafisa hao watakaoteuliwa watakuwa na wakati mgumu.
0 comments:
Post a Comment