Polisi katika mji mkuu wa Somalia
Mogadishu wanasema kuwa wanamgambo wa al-Shabab wamewaua takriban watu 9
wakati wa shambulizi kwenye hoteli moja iliyo karibu na ikulu ya rais.
Ripoti
zinasema kwa mshambuliaji wa kujitolea muhanga aliendesha gari katika
lango la hoteli hiyo kabla ya watu waliokuwa na silaha kuingia ambapo
ufyatulianaji wa risasi ulianza na walinzi wa hoteli.
Kundi la wanamgambo la Al Shabaab linesema kuwa liliendesha shambulizi hilo.
Al
Shabab walikuwa wikidhibiti sehemu nyingi za mji wa Mogadishu kabla ya
kuondoka lakini wanaendesha mashambulizi ya mara kwa mara.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment