Watu zaidi ya 28 wamefariki baada ya
mlipuko mkubwa kutokea katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara Jumatano
jioni, maafisa wa Uturuki wamesema.
Gar lililojaa vilipuzi lililipuliwa mabasi ya jeshi yalipokuwa yakipita, kwa mujibu wa afisi ya gavana wa Ankara.
Mlipuko huo ulitokea karibu na Bunge na makao makuu ya jeshi ya Uturuki.
Naibu waziri mkuu Bekir Bozdag amesema hicho ni “kitendo cha ugaidi”.
Baadhi ya waliofariki na kujeruhiwa walikuwa raia.
Hakuna kundi lililodai kuhusika kufikia sasa.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment