Viongozi
wa muungano wa vyama vya siasa uitwao Umoja wa Rufaa za Wananchi
Tanzania wamewaomba Wazanzibari kukamilisha haki yao ya kupiga kura
katika uchaguzi wa marudio ili wapate viongozi wa kuwaletea maendeleo
Ujumbe
wa watu saba wa umoja huo ukiongozwa na John Shibuda wa Ada Tadea,
ulitoa kauli hiyo jana ulipokutana kwa mazungumzo na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ofisini kwake Vuga Mjini
Zanzibar.
Taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, ilisema ujumbe huo ni
kutoka vyama visivyokuwa na wabunge ambavyo ni UPDP, Sau, UDP na
Ada-Tadea.
Msimamo
wa vyama hivyo unakinzana na ule wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
uliotoa tamko la kususia uchaguzi huo wa marudio.
Kwa
upande wake John Cheyo alisema upigaji kura ndiyo njia pekee itakayotoa
mwanga kwa wananchi wa Zanzibar kuamua wapi wanataka kuelekea katika
mustakabali wa maisha yao ya baadaye.
Wakati
huohuo, vyama 12 visivyo na uwakilishi bungeni vimetoa tamko la
kushiriki uchaguzi huo vikisema hoja za kugomea uchaguzi huo hazina
mashiko.
0 comments:
Post a Comment