Mgombea kiti cha Urais nchini
Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump ametangaza sera zake
kuhusu uhamiaji wakati wa hotuba yake huko Phoenix, Arizona.
Trump
aliwataja watu kadhaa ambao anasema waliuawa na wahamiaji haramu na
kusema kuwa nchi yake ina haki ya kuchagua ni raia gani wa kigeni
wanaruhusiwa kuingia.
Pia aliahidi uhusiano mpya na taifa la Mexico.
Trump ameyasema hayo saa kadha baada ya ziara yake nchini Mexico kwa mazungumzo na Rais Enrique Pena Nieto.
Aidha
amesifu mchango unaotolewa na Wa Marekani wenye asili ya Mexico, lakini
akatetea mpango wake wa kujenga ukuta kati ya nchi hizo mbili.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment