Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewahukumu raia wawili wa China waliokutwa na
hatia ya kuua tembo 226 adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela au kulipa
faini ya Sh108.7 bilioni.
Pia,
imeamuru magari matatu ya washtakiwa hao yenye usajili wa namba T 317
BXG, T 777 BET na T 728 BGP pamoja na vipande 728 vya meno ya tembo
walivyokutwa navyo vitaifishwe na Serikali.
Akitoa
hukumu hiyo jana, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
Cyprian Mkeha alisema katika shtaka la kushawishi askari polisi na
maofisa wa wanyamapori wapokee rushwa ya Sh30.2 milioni ili wasiwapekue
na kuwafikisha katika mikono ya sheria, kila mshtakiwa amehukumiwa
kifungo cha miaka mitano jela ama kulipa faini ya Sh1 milioni.
Akiendelea kusoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha aliwaachia huru washtakiwa hao katika shtaka la kukutwa na ganda la risasi.
Raia
hao wawili wa China, Xu Fujie na Huang Gin waliokuwa wakitetewa na
mawakili, Edward Chuwa na Nehemia Nkoko, waliadhibiwa adhabu hizo baada
ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi tisa wa
upande wa mashtaka pamoja na utetezi wao.
Hakimu
Mkeha alipokuwa akisoma hukumu hiyo, alisema katika shtaka la kukutwa
na vipande 706 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh5.4 bilioni bila ya
kuwa na kibali, kila mshtakiwa anatakiwa alipe fidia ya Sh54.35 bilioni
na kwamba, iwapo watashindwa watumikie kifungo cha miaka 30 jela.
Akiendelea kuisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alisema ametoa adhabu hizo kwa kuzingatia uzito wa maombi ya mawakili wa Serikali, Faraja Nchimbi na Paul Kadushi na maombi ya utetezi ya kutaka wapunguziwe adhabu.
Akiendelea kuisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alisema ametoa adhabu hizo kwa kuzingatia uzito wa maombi ya mawakili wa Serikali, Faraja Nchimbi na Paul Kadushi na maombi ya utetezi ya kutaka wapunguziwe adhabu.
“Kwa
kuzingatia hali halisi ya kesi, ushahidi, hasara ambayo Taifa imeipata
kutokana na Tembo hao 226 waliopoteza maisha kwa kuuawa na washtakiwa ni
wazi washtakiwa walitishia maisha ya vizazi vya tembo waliomo ndani ya
mipaka ya nchi yetu,” alisema Hakimu Mkeha.
Alisema
ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka
kwa kuwa umethibitishwa pasipo kuacha shaka yoyote.
Kwa
upande wa Mawakili wa Serikali, Nchimbi aliiomba Mahakama iwape adhabu
kali washtakiwa hao kwa kuwa kati ya kipindi cha 2010 na Desemba 2013,
jumla ya tembo 892 waliuawa nchini.
Alisema
washtakiwa hao waliingia nchini 2010 hadi Novemba 2013 walipokamatwa
kwa makosa hayo na kuwapo kwao rumande, matukio ya mauaji ya tembo
yalipungua.
Nchimbi
alibainisha kuwa washtakiwa hao waliua robo ya tembo wanaouawa hapa
nchini na kwamba, kutokana na wingi wa nyara walizokutwa nazo,
inaonekana wazi ni miongoni mwa vinara, wawezeshaji na wahusika wa
shughuli za ujangili zinazoendelea nchini.
Alisisitiza kuomba wapewe adhabu kali kwa kuwa tembo ni miongoni mwa wanyama watano wanaoongeza mapato la Taifa kupitia utalii.
Wakili wa utetezi, Nkoko aliiomba Mahakama iwapunguzie adhabu wateja wao kwa kuwa walikwisha kaa rumande miaka mitatu.
Washtakiwa
hawa walikamatwa na nyara hizo za Serikali na aliyekuwa Waziri wa
Wizara ya Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki.
Wakati
wa usikilizwaji wa kesi hiyo, upande wa mashtaka ukiendeshwa na Wakili
wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, uliwaita mashahidi tisa wakiwamo
wapelelezi, majirani wa washtakiwa walioshuhudia upekuzi, maofisa kutoka
polisi na Wizara ya Maliasili na Utalii ambao walitoa ushahidi dhidi ya
washtakiwa hao.
Miongoni
mwa ushahidi wao, walidai kuwa Oktoba 20, 2013, walipokea taarifa kuwa
kuna meno ya tembo yanasafirishwa kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara na
Ruvuma kwenda Dar es Salaam na yangeuzwa eneo la Biafra Kinondoni, Dar
es Salaam.
Walidai
kuwa Novemba 2,2013, waliona gari likiendeshwa na raia hao wa China
walilifuatilia hadi kubaini shehena hizo za meno ya tembo
zilipohifadhiwa.
0 comments:
Post a Comment