Gazeti moja nchini Marekani linasema
kuwa limepata nyaraka zinazoonyesha kuwa Donald Trump alikuwa
ametangaza kupata hasara ya zaidi ya dola milioni 900 mwaka 1995.
Gazeti
la The New York Times linasema kwa hasara hiyo ilikuwa kubwa zaidi na
ingemwezesha mgombea huyo wa urais wa chama cha Republican kutolipa
ushuru kwa zaidi ya miaka 18 kisheria.
Kampeni ya bwana Trump ambayo imekataa kutoa rekodi zake za ushuru na haikukubali wala kukana hasara ambazo Trump amepata.
Katika
taarifa imesema kuwa Trump ni mfanyibiashara hodari ambaye alijua
sheria kuhusu ulipaji ushuru zaidi ya mtu yeyote yule ambaye amewahi
kgombea urais.
0 comments:
Post a Comment