Zikiwa zimepita siku mbili toka kupatikana kwa Katibu Mkuu mpya wa CHADEMA Dk Vincent Mashinji, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla ameibuka na kuwapa pole CHADEMA kama walimchagua Katibu Mkuu wao kwa kuangalia historia yake.
Kupitia
Account yake ya Facebook Dk Hamisi Kigwangalla anakiri wazi kuwa Dkt.
Mashinji ni msomi mzuri na mwanasiasa mzuri ingawa anadai hana uhakika
kama alimaliza masomo ya ubingwa.
"Ndg.,
Dkt. Mashinji is a friend, brother and colleague. Hakuwahi kutuokoa
mimi na Dkt. Ulimboka, na hakuwahi kuongoza mgomo, sema alishiriki mgomo
ulioongozwa na mimi na Dkt. Ulimboka.
"Kiukweli,
ni mwanasiasa mzuri, msemaji, msomi mzuri (tumesoma naye MBA chuo
kimoja), sina hakika kama alimaliza masomo ya Ubingwa maana alinyanyaswa
na Supervisor wake, akasusa akaamua kujiiunga masomo ya MBA na sina
hakika sana kuhusu 'msimamo usiotetereka'.
"Maana
baada ya vitisho vya 2005, aliyumba sana na tulimtenga na ku-aVoiD
kumualika vikao vya CC ya mgomo. Hivyo, kama kigeZo kilikuwa ni hii
historia, pole kwa CHADEMA." Ameandika Dk Kigwangalla.
0 comments:
Post a Comment