CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetuma salamu za rambirambi
kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wake wa Viti Maalum, Leticia Nyerere
kilichotokea juzi nchini Marekani.
Leticia
alifariki dunia katika hospitali ya Doctors Community iliyopo Lan ham,
Maryland Jumapili saa 2 usiku wa saa za Afrika Mashariki alikokuwa
amelazwa kwa matibabu.
Taarifa
ya Chadema iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa
chama hicho, Tumaini Makene ilisema kuwa chama hicho kimepokea kwa
masikitiko makubwa msiba wa Leticia Nyerere uliotokea nchini Marekani.
“Tunatoa
pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki katika wakati huu mgumu wa
kuondokewa na mpendwa wao, Mwenyezi Mungu awatie moyo wa ujasiri na
subira katika wakati huu mgumu wa majonzi ya msiba huo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya Makene.
Makene
alisema Chadema watamkumbuka Leticia kwa mchango wake na ushiriki wake
wakati wote alipokuwa mwanachama wao na akiwa miongoni mwa watu
waliopata fursa za kuwa wabunge kupitia Chadema.
Msemaji
wa familia ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku juzi alimueleza Rais
Magufuli kuwa familia inaendelea na taratibu za kuusafirisha mwili wa
marehemu kutoka nchini Marekani kuurejesha nyumbani kwa maziko.
0 comments:
Post a Comment