Rais John Magufuli
amewataka watu walioficha fedha majumbani kuziachia ziingie kwenye
mzunguko vinginevyo anaweza kuamua kuzibadili ili wakose mahali pa
kuzipeleka.
Amesema watu hao wamekuwa na utaratibu wa kutoa fedha zao katika benki na kuzificha kwa kuogopa kuwa atabaini kiasi walichonacho, hivyo akawataka kuachana na tabia hiyo kwa sababu fedha hizo ni mali yao.
Akizungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika
katika Ukumbi wa Mlimani City jana, Rais Magufuli aliyetumia dakika 73
kuzungumza na wahandisi hao na kueleza mikakati na changamoto
zinazoikabili Serikali ukiwamo wizi na ufisadi, alisisitiza;
“Huu ujumbe ni kwa wale wanaoficha fedha, waziachie na wajiandae, naweza kuamua baada ya siku mbili tatu nabadilisha fedha na hizo zilizofichwa katika magodoro ziozee huko. Ni nafuu mzitoe mziweke katika mzunguko zikafanye kazi,” alisema.
“Huu ujumbe ni kwa wale wanaoficha fedha, waziachie na wajiandae, naweza kuamua baada ya siku mbili tatu nabadilisha fedha na hizo zilizofichwa katika magodoro ziozee huko. Ni nafuu mzitoe mziweke katika mzunguko zikafanye kazi,” alisema.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na mawaziri, naibu
mawaziri, makatibu wakuu na wahandisi kutoka ndani na nje ya nchi, Rais
Magufuli alisema katika utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano hakuna
fedha za bure.
Alibainisha kuwa kipindi cha nyuma, fedha zilikuwa nyingi
mitaani kwa sababu baadhi ya watu walikuwa wakiiba fedha za Serikali,
huku akitoa mfano wa jinsi mabilioni ya fedha za watumishi hewa
yalivyotafunwa, jambo alilosema sasa limedhibitiwa.
“Nyinyi wahandisi ni
wachapa kazi, huu ndiyo wakati wa kutajirika.Tumieni nafasi hii maana
watu walizoea kupata fedha za bure. Waliokuwa wanatafuta dili katika
wizara hawapati kitu na sasa nikijua mtendaji wa Serikali umepiga dili
utaondoka tu,” alisema.
“Fedha za bure hazipo na ndiyo maana thamani ya
nchi na fedha yetu imeanza kuongezeka na mfumuko wa bei umeshuka mpaka
asilimia 5.1.”
Alisema wakati fulani akiwa anatoka mkoani Geita, mfuko
wa saruji ulikuwa unauzwa Sh26,000 lakini sasa unauzwa Sh16,000.
"Wanaoficha fedha ni wachache. Watu watapata fedha za kutosha kwa kufanya
kazi. Wafikirie kufanya uwekezaji wa viwanda vyao na nyinyi wahandisi
muwe namba moja.”
Changamoto na mikakati ya serikali yake
Alisema licha ya Serikali
kuamua kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka 87,000 hadi
137,000, imebainika kuwa wilaya moja mkoani Arusha ina wanafunzi hewa
zaidi ya 10,000 na wilaya nyingine iliyopo Mwanza ina wanafunzi hewa
zaidi ya 8,000.
Kuhusu mapato ya Serikali, alisema baada ya kuingia
madarakani yalipanda kutoka Sh800 bilioni hadi Sh1.3 trilioni lakini
wakati hayo yanafanyika, Serikali imebaini wafanyakazi hewa zaidi ya
16,500 na kusema hiyo ndiyo Tanzana aliyoikuta.
Rais Magufuli pia
alieleza mikakati ya kununua meli mbili, kujenga reli ya kisasa,
kukarabati viwanja vya ndege na kufafanua sababu za Serikali kununua
ndege mbili aina ya Bombadier Q400, ambazo zimeshalipiwa asilimia 40.
“Hizi ndege hazili mafuta, kasi yake nzuri, zinatua uwanja wowote hata
wa changarawe. Wapo wanaoziponda eti hazina kasi, kama unataka kasi
kapande za jeshi,” alisema huku akicheka.
Huku akieleza jinsi wahandisi
wa nje wanavyotekeleza
miradi kwa gharama kubwa, alisema katika bajeti ya mwaka 2016/17,
Serikali ilitumia Sh100 bilioni kwa ajili ya kukarabati viwanja saba vya
ndege vya lami, lakini wapo waliotumia Sh105 bilioni kujenga barabara
ya kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa Ndege Mwanza, fedha ambazo ni
nyingi.
“Uwanja wa ndege Dar es Salaam unaokarabatiwa sasa, zimejengwa
njia tatu (za kuruka ndege) na lile jengo (la abiria) lakini zimetumia
Sh650 bilioni na gharama hizo zimewekwa na wahandisi. Tunahitaji kufanya
uchunguzi, maana gharama hizi ni kubwa sana, kwa nini Watanzania
tunachezewa hivi?” alihoji na kuongeza, “Ni bora wangepewa wahandisi wa
Tanzania wakala hizi hela.”
Alisema wahandisi wazawa wanaweza kujipanga na kupata tenda ya kujenga reli ya kisasa, kujenga bomba la gesi
kutoka Tanga kwenda Uganda na hata kujenga viwanja vya ndege.
Wizi unavyofanyika sekta
ya madini
Alisema katika sekta ya madini, nchi inaibiwa na kutoa
mfano jinsi dhahabu inavyochimbwa wilayani Kahama, kisha wahusika
kuchukua mchanga na kwenda nao nje ya nchi kwa ajili ya kusafishwa.
“Kinachosafishwa
huko nje hatujawahi kukiona, wahandisi mmekaa kimya. Kuna uhakika gani
katika kontena kama hakuna kilo 200 za dhahabu ambazo
wameziyeyusha na kuzichanganya na mchanga? Hivi wahandisi tumeshindwa
kuweka utaratibu wa kubaini kilichomo katika mchanga? Tunashangilia mtu
anasafirisha mchanga na sisi tunakubali kuwa wanasafirisha mchanga,
mchanga unaondoka na viongozi wetu hata majeshi yetu na polisi
unasindikiza mali yako.”
Alisema suala hilo pia linapaswa kuwa
changamoto kwa viongozi na wanasiasa na akahoji sababu za kila mgodi wa
dhahabu kuwa na uwanja wa ndege,
“Tena hizi ndege wakati mwingine
zinaruka moja kwa moja. Sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana.
“Nasikia
Profesa Muhongo (Sospeter – Waziri wa Nishati na Madini) atatoa mada
katika mkutano huu, atueleze kwa namna gani mchanga wetu utaacha
kupelekwa nje? Katika vitu vinavyoniumiza ni pamoja na hili. Haya
mamchanga tuyashike tuangalie kilichomo humo ndani. Tanzania tumechezewa
na kuibiwa mno, nipo serikalini najua. Kila mahali ni dili, ukigeuka
huku dili, ukienda huku dili, kila mahali ni dili tu,” alisema.
Siri ya
kuteua wahandisi wengi serikalini
Rais Magufuli alisema, wakati akiomba kura katika
kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita, alinadi mkakati wa kuifanya Tanzania
kuwa nchi ya viwanda, lakini hakuwahi kusema watu watakaomsaidia kwa
sababu aliamini wahandisi hawatamtupa mkono katika kufanikisha hilo.
Huku akifichua siri ya kujaza wahandisi katika serikali yake, alisema
taaluma hiyo ni muhimu katika maendeleo ya nchi na kuwataka kuwatumia
viongozi hao kujenga uchumi wa Taifa, ikiwa ni pamoja na kuanzisha
viwanda.
“Tusipotumia wahandisi kamwe tusizungumze kuhusu maendeleo ya
nchi yetu, tusahau. Nimeteua wahandisi kutekeleza mambo kwa niaba ya
wahandisi. Mnatumika kujenga uchumi wa watu wengine. Jipangeni nawaunga
mkono, anzisheni viwanda… kampuni zenu na kupata kazi maana hakuna nchi
duniani isiyotaka kujenga watu wake,” alisema. ...
0 comments:
Post a Comment