Uongozi
wa Studio ya Muziki ya The Industry iliyoko chini ya Wanamuziki
Producer Nahreel na Aika Marealle unapenda kuchukua Nafasi hii
kuwatangazia Umma Kuwa kuanzia Tarehe 14 January 2016 Wamemuingiza
Msanii mpya wa Kike aitwaye Rosa Ree, Rose Ree ni muimbaji wa Muziki
aina ya Rap ambae kazi zake zitaanza kusikika/Kuonekana siku si nyingi
kuanzia sasa katika Redio Mbali mbali na TV Stations za Tanzania na nje
ya nchi.
Kama
wasikilizaji na watazamani tunaomba Kumuunga mkono Msanii huyu mpya
Kwani tuna uhakika hatawaangusha katika kuwaletea burudani Katika
Masikio na macho yenu pindi kazi zake zitakapoanza kutolewa hivi
karibuni.
The
Industry ni studio na kampuni ya muziki ambayo ipo chini ya kundi la
music lenye Mafanikio makubwa la Navy Kenzo ikisimamiwa na Producer
Nahreel na msaidizi wake Aika Marealle
Wasanii
Baadhi Waliokwisha fanya kazi na Studio ya The Industry mpaka sasa toka
kuanzishwa kwake hivi karibuni ni Diamond Platnumz na wimbo wake wa
Nana, Nikki wa Pili na wimbo wa Baba Swalehe, Joh Makini na nyimbo zake
kama Don’t Bother na nusu nusu.
Imetolewa na,
The Industry PR
John Kiandika
0 comments:
Post a Comment