Jaji mmoja katika jimbo la
Carlifonia nchini Marekani ameiamrisha kampuni kubwa ya Teknolojia ya
Apple kusaidia polisi katika kuchunguza simu ya mwanamume ambaye
aliwapiga risasi watu 14 katika eneo la San Bernardino mwezi Disemba.
Syed Rizwan Farook na mkewe waliuawa na polisi baada ya kisa hicho.
Jaji
alisema kuwa kampuni ya Apple ni lazima itoe msaada wa kiteknolojia
baada kushindwa kuweka nywila ya simu hiyo kwa mara kumi. Kampuni hiyo
bado haijatoa tamka lolote na ina muda wa siku tano kupinga uamuzi huo.
Tangu
kutolewa kwa programu mnamo mwezi Septemba 2014,data ya simu za Apple
kama vile ujumbe na picha zimewekewa usalama wa kutosha.
Hii ina
maanisha kwamba iwapo simu hiyo imefungwa ,ni nywila au neno la siri la
simu hiyo linaloweza kuifungua na kupata data hiyo.
Iwapo mtu atajaribu mara 10 bila mafanikio data iliopo ndani ya simu hiyo hujifuta .
Hakuna
mtu ama hata kampuni ya Apple itaweza kupata ujumbe huo,hatua ambayo
kampuni hiyo ilifanya kufuatia ufichuzi wa bwana Edward Snowden kwamba
serikali ya Marekani imekuwa ikidukua simu za raia.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment