Mwalimu mmoja kutoka Kenya ni
miongoni mwa walimu wengine kumi waliofuzu fainali ya waliorodheshwa
kuwania tuzo ya mwalimu bora katika harakati zake za kukabiliana na
itikadi kali.
Ayub Mohammed ni mwalimu wa somo la biashara na lile la dini la IRE katika shule ya upili ya Eastleigh mjini Nairobi.
Tuzo
hiyo ya dunia ilioanzishwa na hazina ya fedha ya Verkey,ikiwa ni
shirika la hisani la kampuni ya kimataifa ya elimu ya Gems,inayolenga
kutafuta habari za mashujaa wanaobadilisha maisha ya vijana.
Amekuwa akijenga mtandao wa walimu walio na maono kama yake na kutengeza utaratibu unaolenga kukabiliana na itikadi kali.
Tuzo hiyo ilipata maombi kutoka kwa walimu katika mataifa 148.
Mshindi ambaye atatangazwa mwezi Machi ,atapokea dola milioni moja.
Walioorodheshwa
ni pamoja na Aqeela Asifi,ambaye anawafunza wakimbizi nchini Pakistan
na Hana Al Hroub ambaye alilewa katika kambi moja ya wakimbzi nchini
Palestina na ambaye sasa ni mwalimu.
Mshindi wa tuzo hiyo mwaka jana alikuwa Ancie Atwell kutoka Marekani ambaye alitoa fedha hizo kwa shule yake.
Tuzo
hizo zilitolewa katika sherehe iliohudhuriwa na aliyekuwa rais wa
Marekani Bill Clinton huku Bill Gates akitoa mchango wake.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment