Mgombea wa urais wa chama cha
Republican Donald Trump ameshinda katika jimbo la Nevada nchini
Marekani, na hivyobasi kuimarisha uongozi wake katika mchujo wa kuwania
tiketi ya chama hicho.
Tajiri huyo sasa ameshinda mara tatu ,kufuatia ushindi wake katika jimbo la New Hampshire na Carolina kusini.
Seneta Marco Rubio na Ted Cruz ambao wamekuwa wakishambuliana wiki hii wanapigania nafasi ya pili.
Maafisa
wa chama hicho wamesema wamekuwa wakichunguza ripoti za watu kupiga
kura mara mbili huku eneo moja likidaiwa kuwa na vifaa vichache vya
kupigia kura.
Baadhi ya watu waliojitolea pia walidaiwa kuvaa nguo
zenye picha za bwana Trump,lakini maafisa wamesema kuwa hatua hiyo sio
kinyume na sheria.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment