Syria imesema kwamba mashambulio ya
anga yanayofanywa na Uturuki katika maeneo ya Syria ambayo hivi karibuni
yaliingia katika himaya ya wapiganaji wa kikurd ni ukiukaji wa mipaka
ya nchi hiyo, na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua
hatua.
Vile vile imeituhumu Ankara kwa kuruhusu watu takriban mia moja wenye silaha kuingia nchini Syria. Peter Mfalila na maelezo zaidi:
Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amesema mashambulizi hayo katika maeneo ya wakurd mpakani na Syria yataendelea.
Kwa upande wake Ankara imesema, kundi la kikurd la PYD linahusishwa na wapiganaji wa PKK ambao kwa miongo kadhaa wamekuwa wakifanya kampeni dhidi ya Uturuki. Hata hivyo, Marekani haikubaliani na mtizamo wa Ankara, huku ikiliona kundi la PYD kama mshirika mkubwa katika mapambano dhidi ya wapiganaji wa Islamic State nchini Syria.
Nae waziri mkuu wa Urusi, Dmitry Medvedev ameionya Marekani kwamba kupelekwa kwa vikosi nchini Syria kutasababisha kuwepo kwa vita kamili.
Medvedev alikuwa akijibu kauli iliyotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ambae amesema iwapo jitihada za kuleta amani nchini Syria hazitafanikiwa, basi vikosi vya kigeni zaidi zinaweza kuingia nchini humo.
Kauli hiyo ameitoa katika mahojiano na televisheni ya Euronews . Makubaliano sharti yafikiwe kwa njia ile ile kama ilivyokuwa katika mazungumzo ya Kerry na Lavrov, badala ya kusema kwamba mambo yakiharibika, nchi nyingine za kiarabu na Marekani wataendesha operesheni ya kijeshi ardhini.
Nimejibu suala hili hivi karibuni. Lakini ngoja nirudie tena kwamba hakuna mtu anataka vita, lakini vikosi vya ardhini ni vita kamili vya muda mrefu. Lazima tujue hilo.
0 comments:
Post a Comment