Adverts

Thursday, February 25, 2016

Mfuko wa Habari Tanzania (TMF ) Wasema Uko Tayari Kutoa Msaada wa Fedha Ili Kuiwezesha TBC Kutangaza LIVE Mwenendo wa Bunge


Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko  wa  Habari Tanzania (TMF) Ernest Sungura amesema taasisi yake iko tayari kugharamia matangazo ya  live Bungeni  kupitia TBC  ili  kuwawezesha  wananchi  kujua  kinachoendelea  Bungeni.

Akizungumza leo jijini  Dar  es  Salaam katika mkutano na wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari nchini mbele ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari( MAELEZO), Assah Mwambene, Sungura  amesema lengo la TMF ni kuleta mabadiliko chanya  katika tasnia ya habari na kuona wananchi wanapata taarifa kwa wakati.

0 comments:

Post a Comment