Rais
wa Uganda Yoweri Museveni amesema kwamba ameandaa mrithi wa shamba lake
lakini sio mrithi wa Uganda na Waganda watachagua mtu wa kuwaongoza
pale ambapo yeye atastaafu wadhifa huo.
Museveni
ameyasema hayo kipindi ambapo kampeni za lala salama zinaendelea nchini
Uganda na uchaguzi wa kumpata Rais wa nchi hiyo unafanyika siku ya
Alhamisi ya wiki hii.
Rais
Museveni ambaye amedumu madarakani kwa muda wa miaka 30 anatetea tena
nafasi yake hiyo huku akitamba kuwa hakuna chama chenye uwezo wa kuweza
kushinda chama chake cha National Resistance Movement (NRM)
“Sidhani
vyama vya upinzani vitashinda NRM. Kwa sababu tunajua nguvu yetu.
Tunajua tutashinda, lakini kama itakuwa tumeshindwa basi tutawaachia
wale ambao wameshinda. Lakini sidhani kuna chama kinaweza kushinda NRM
wakati huu,” amesema
Aidha
kwa sasa katiba inaeleza umri wa juu zaidi wa Rais kuwa madarakani ni
miaka 75. Kwa sasa Rais Museveni anakaribia kutimiza umri wa miaka 72
ikimaanisha kwamba katika mwaka wake wa mwisho wa muhula ujao iwapo
ataingia madarakani, atakuwa na umri wa miaka 76.
Chanzo BBC
0 comments:
Post a Comment