Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watu wawili kwa
tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo
moja, akiwamo anayedaiwa kuwa kigogo wa biashara ya dawa hizo nchini.
Kamanda
wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa
habari jana kuwa, juzi saa 1.15 usiku katika maeneo ya Mbezi Beach,
walimkamata mtuhumiwa wa kwanza akiwa na gari baada ya kumpekua alikutwa
na dawa hizo za kulevya.
Alisema walipomhoji zaidi, alidai kuwa dawa
hizo siyo zake, bali za tajiri yake anayeishi Mikocheni jijini hapa
ambaye wali panga kukutana naye maeneo ya Mbezi Beach kwa ajili ya
kukabidhiana.
Alisema upelelezi unaendelea na utakapokamilika,
watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
Kukamatwa kwa kigogo huyo na
msaidizi wake ni mafanikio ya jeshi hilo ambalo hivi karibuni
lilimkamata kigogo mwingine muuza ‘unga’ jijini hapa hivi karibuni.
Wakati
huohuo,Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kupitia kitengo
chake cha usalama Barabarani limekamata magari mbalimbali kwa makosa ya
usalama barabarani
Kamanda Sirro amewataka madereva kuwa makini na waangalifu pindi wawapo barabarani ili kuepuka adhabu zitolewazo ili vipato hivyo viwasaidie katika maisha yao ya kila siku.
0 comments:
Post a Comment