Waziri
wa Elimu Sayansi, Teknolojia na ufundi, Prof Joyce Ndalichako
amesitisha mkataba wa kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo George Nyatenga (Pichani chini).
Pia
amewasimamisha kazi wakurugezi watatu wa Bodi hiyo ambao ni Mkurugenzi
wa Fedha na Utawala Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo Juma
Chagonja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo.
Prof
Ndalichako amemwagiza Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali ahakiki
maelezo na Nyaraka zilizowasiliwa na Bodi ya Mikopo pamoja na kufanya
ukaguzi maalum kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi sasa.
0 comments:
Post a Comment