SERIKALI
imesema Tanzania haitajitoa katika Mahakama ya Kimataifa yaMakosa ya
Jinai (ICC). Hata hivyo, imesema tabia ya ubaguzi dhidi ya viongozi wa
Bara la Afrika inayooneshwa na mahakama hiyo inaweza kurekebishwa.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk Agustine Mahiga wakati
akizungumza na waandishi wa habari juu ya Siku 100 za Rais John Magufuli
tangu aingie madarakani.
“Sisi
ni miongoni mwa nchi ambazo zimesaini mkataba wa Roma ambao ulianzisha
Mahakama ya ICC… Tunataka kuona baadhi ya mambo yakirekebishwa ili
kuondoa kile kinachoonekana kuwa ni ubaguzi kwa viongozi wa Afrika,” alisema Balozi Mahiga.
Waziri
huyo alisema, katika Siku 100 za Serikali ya Awamu ya Tano Tanzania
imeweza kufanikiwa katika mambo mengi kupitia Wizara hiyo ikiwa ni
pamoja na kushughulikia masuala ya uhusiano na migogoro mbalimbali.
Alisema
tangu alipoapishwa kuwa Waziri ameshughulikia baadhi ya migogoro
ukiwemo wa Burundi ambapo Rais Magufuli alimuagiza kwenda nchini humo
ili kuzungumza na Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza ili akubali
kufanya mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa mgogoro unaoendelea nchini
mwake.
Balozi
Mahiga alisema, hatua ya Rais kuzuia safari za nje kwa watumishi
imesaidia kupunguza gharama ambazo wakati mwingine zilikuwa si za
lazima, hivyo ni jambo ambalo linapaswa kupongezwa.
“Si
kwamba Rais hatasafiri, hapana ila kwa sasa tunajua bado ana jukumu
kubwa la kujenga serikali yake. Serikali si kwa maana ya Mawaziri tu ila
watendaji wote kwa ujumla. Mambo yakishatulia nadhani hata yeye sasa
ataweza kusafiri kwa safari atakazohitajika,” alisema.
0 comments:
Post a Comment