Wanasayansi wa Marekani wanachunguza uhusiano kati ya virusi vya Zika na hali ya watoto kuzaliwa na vichwa vidogo |
Wanasayansi kutoka kituo cha
kudhibiti na kuzuia magonjwa CDC nchini Marekani wameanza kufaya utafiti
nchini Brazil ili kujua uhusiano kati ya Virusi vya Zika na watoto
kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo.
Timu za wanasayansi zimekuwepo
katika jimbo la paraeeba,kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, jimbo ambalo
limeathirika zaidi na Virusi.
Timu nane zinazoundwa na cdc na
mawakala wa maswala ya afya walienda kwenye maeneo yaliyoathirika na
kuchukua sampuli ya damu na kuwahoji wamama walioathirika na wamama
ambao watoto wao walizaliwa wakiwa na vichwa vidogo.
Katika
kipindi cha majuma yajayo, watakusanya taarifa kutoka kwa mamia ya
wamama katika jimbo la paraeeba, jimbo la pili lililoathirika zaidi.
Katika
Ripoti ya siku ya jumanne Wizara ya Afya ya Brazil imethibitisha watoto
587 wana vichwa vidogo.asilimia 75 zaidi ya wiki iliyopita huku maelfu
ya watoto wanachunguzwa.
Baada ya kutangazwa hali ya taadhari ya
kiafya, Rais wa Shirika la Afya duniani, Margaret Chan aliwasili
Brasilia kufuatilia hali ilivyo.
Akiwa huko alikutana Rais wa
Brazil,Dilma Roussef siku ya jumanne na kusema kuwa anafurahishwa na
namna Serikali inavyoshughulikia tatizo hilo na kutaka jamii isaidiwe
kupambana na mbu anayeeneza virusi vya Zika.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment