Waziri
wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati)
akizungumza na waandishi wa Habari leo hii katika ofisi za Baraza la
Michezo la Taifa (BMT) na kutengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mtendaji
mkuu wa baraza ilo Bw. Henry Lihaya (wa kwanza kushoto) leo jijini Dar
es Salaam kutokana utendaji usiolizisha. Picha na Daudi Manongi.
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ametengua
uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania Henry Lihaya
baada ya kushindwa kutekeleza wajibu wake.
Mhe.
Nnauye ametengua uteuzi huo katika ziara yake aliyoifanya leo mapema
katika ofisi za BMT kuona miundo mbinu ya ofisi hizo na kujua changamoto
walizonazo.
“Baraza likirekebishwa vyama vya michezo navyo vitakuwa mguu sawa na kuleta chachu na maendeleo katika michezo,”alisema Mhe. Nnauye.
Aliongeza
kwa kusema kuwa, miaka saba ambayo Lihaya amekuwa Katibu Mtendaji wa
Baraza imetosha kwani hakuna mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika sekta
ya michezo tangu alipoteuliwa mwaka 2009.
Kutokana
na utenguzi huo Mhe. Nnauye amemtaka Mwenyekiti wa BMT Dionis Malinzi
kupendekeza jina la Katibu Mtendaji mpya wa BMT ambaye anampendekeza kwa
mujibu wa sheria ya BMT kifungu cha 5(1) baada ya kupata idhini ya
waziri mwenye dhamana.
Vilevile,
Mhe. Nnauye amemtaka mwenyekiti kuteua Katibu Mtendaji ambaye atakuwa
ni mchapa kazi na mwenye mipango ambayo itaibadilisha BMT na kuleta
chachu katika michezo nchini.
Aidha,
Mhe. Nnauye amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara ya habari, utamaduni sanaa
na michezo kumpangia Lihaya kazi nyingine wizarani.
0 comments:
Post a Comment