Mkazi
wa Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora, Mashaka Maziku (60) amehukumiwa
kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la kumkata sehemu za siri mkewe
kwa imani za kishirikina ili apate mali.
Hakimu
Joctan Rushwela alisema jana kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa
Tabora imeridhishwa na ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka.
Hakimu
Rushwela alisema anamhukumu mshtakiwa huyo kwenda jela ili iwe fundisho
kwa wengine wanaokuwa na tamaa ya kujipatia mali kwa njia za
kishirikina.
Awali
wakili wa Serikali, Idd Mgeni alidai kuwa mshtakiwa huyo na mganga wa
jadi, walitenda kosa hilo kati ya Oktoba 29 na Novemba 2, 2014 katika
eneo la Kazaroho Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora.
Wakati
wa tukio hilo, ilidaiwa kuwa Maziku aliambiwa na mganga huyo ambaye ni
mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Kahele Paul kwamba akipeleka sehemu
za siri za mkewe atapata Sh5milioni.
Alidai baada ya kupewa ushauri huo, alimchukua mkewe na kwenda kumnywesha pombe ili aweze kutimiza ukatili huo.
Alidai
baada ya kunywa pombe nyingi, alichukua kisu na kumkata sehemu za siri
mkewe na kuzihifadhi kwenye mfuko wa suruali yake na kutoweka.
Alidai
kwa mujibu wa mashahidi wanne, mwanamke huyo alikuwa akipiga kelele
kutokana na maumivu makali aliyopata huku akivuja damu nyingi.
0 comments:
Post a Comment