WAZIRI
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako
ameingilia kati mgogoro wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Joseph Dar es
Salaam, waliogomea kufanya mitihani na kuwataka warejee madarasani
wakati matatizo yao yakishughulikiwa.
Wanafunzi
hao walikuwa katika siku ya tatu ya mgomo wao jana ambapo pamoja na
mambo mengine walikuwa wakilalamikia mapungufu yaliyopo chuoni hapo,
ikiwa ni pamoja na maabara za kufanyia mafunzo kwa vitendo, matatizo ya
kiutawala, mitaala ya kufundishia pamoja na ada.
Profesa
Ndalichako aliwasili chuoni hapo jana asubuhi na kukagua mazingira ya
kufundishia ya chuo hicho kwa kutembelea maabara zote chuoni hapo na
kisha kwenda kuzungumza na utawala, Serikali ya wanafunzi na mwisho
alihutubia wanafunzi wote.
Ndalichako
baada ya kuzungumza na pande zote mbili aliagiza wanafunzi hao warejee
madarasani kuendelea na mitihani yao na kuutaka uongozi wa chuo
uyafanyie marekebisho mapungufu ya kiutawala yaliyojitokeza.
Aidha
ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), chini ya Katibu Mtendaji
wake, Profesa Yunus Mgaya kufuatilia na kuchunguza kwa makini madai ya
wanafunzi hao juu ya kuwepo kwa wahadhiri wasio na sifa zinazotakiwa.
0 comments:
Post a Comment