Baada ya Dk Ali Mohammed Shein kutangazwa mshindi kwa zaidi ya asilimia 90, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hatma ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa itaamuliwa na Rais kwa kufuata matakwa ya Katiba ya Zanzibar.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM,
Waride Bajari Jabu alisema Dk Shein ataongozwa na Katiba ya Zanzibar
pamoja na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika
mkutano huo ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya kumpongeza Dk Shein
kuchaguliwa tena kwa mara ya pili na wananchi wa Zanzibar, Jabu alisema
maelekezo yote ya kuundwa kwa SUK yamefafanuliwa kikatiba.
Alisema
CCM inaamini kuwa katiba ndiyo msingi wa uendeshaji wa nchi, hivyo
jambo ilo wanaliachia liamuliwe kwa kufuata matakwa husika ya Katiba ya
Zanzibar.
“Rais ataunda serikali yake kikatiba, imefafanua kila kitu,” alisema Jabu wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 inataka Serikali inayoundwa iwe ya umoja wa kitaifa kwa kuwa na Rais, Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye anatoka chama kikubwa cha upinzani na Makamu wa Pili wa Rais anayeteuliwa kutoka katika miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 inataka Serikali inayoundwa iwe ya umoja wa kitaifa kwa kuwa na Rais, Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye anatoka chama kikubwa cha upinzani na Makamu wa Pili wa Rais anayeteuliwa kutoka katika miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Hata
hivyo, katika uchaguzi uliofanyika Jumapili, CCM imeshinda majimbo yote
ya uchaguzi kutokana na hatua ya Chama cha Wananchi (CUF) kutangaza
kutoshiriki katika uchaguzi huo wa marudio.
Dk
Shein alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata asilimia 91.4 na mgombea
aliyemfuatia ni wa ADC, Hamad Rashid Mohamed aliyeambulia asilimia tatu
ya kura zilizopigwa.
Kutokana
na kutokuwepo mgombea urais aliyepata zaidi ya asilimia 10 ya kura za
urais na kutokuwepo kwa chama kilichoingiza wajumbe wengi Baraza la
Wawakilishi, CCM imejikuta inabaki pekee yenye sifa zote kikatiba.
Jabu pia alituma salamu za pongeza kwa Dk Shein kwa kuchaguliwa tena kuwatumikia Wazanzibari kwa kipindi cha miaka mitano.
Akitoa
salamu hizo, Jabu alisema ushindi wa Dk Shein umedhihirisha namna
Wazanzibari wanavyoridhishwa na utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na
kumuamini kwao.
Kwa
upande wao, Umoja wa Vijana (UVCCM) umesema ushindi alioupata Dk Shein
ni kielelezo cha kuimarika kwa msingi ya demokrasia Zanzibar na
kukubalika kwa mgombea huyo kwa wapiga kura na wananchi wa Zanzibar.
Kaimu
Katibu Mkuu alisema aina ya uongozi wa Rais Dk Shein ni wa kipekee na
kwamba kama angekuwa si mtawala mwenye maarifa mapana na uvumilivu wa
kisiasa serikali hiyo anaamini ingevunjika mapema.
0 comments:
Post a Comment