Mkutano ulipangwa kufanyika katika
jimbo la Chicago nchini Marekani wa mgombea wa chama cha Republican
Donald Trump umehairishwa baada ya kutokea maandamano.
Mapema polisi waliwakamata zaidi ya watu 30 katika mkutano wa Trump katika jimbo la Missouri.
Ndani ya ukumbi wa mkutano huo vita vilizuka kati ya wafuasi wa na waandamanaji ambao walipeperusha bendera na kutoa matamshi.
Taarifa kutoka kampeni ya bwana Trump ilisema kuwa mgombea huo aliamua kufutilia mbali mkutano huo baada ya kukutana na maafisa wa polisi.
Katika mkutano huo kulikuwa na matamshi ya kumsifu bwana Trump kutoka kwa wafuasi wake huku baadhi ya waandamanaji wakitoa matamshi ya kumsifu Bernie Sanders.
0 comments:
Post a Comment