Mwanafunzi
wa Shule ya Sekondari Mnero iliyopo Tarafa ya Ruponda mkoani Lindi,
ameuawa kwa kunyongwa baada ya kubakwa na wanaume wasiofahamika kisha
mwili wake kutelekezwa kichakani.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga alisema jana kuwa mwanafunzi
huyo alikuwa na tabia ya kuruka ukuta usiku na kwenda nje ya shule
kufuata wanaume.
Kamanda
Mzinga alisema mwanafunzi huyo alipofika kwenye kichaka hicho kilichopo
karibu na eneo la Kanisa Katoliki alibakwa na wanaume hao kisha kumuua
kwa kumnyonga.
Alisema wanamshikilia mwendesha bodaboda, mkazi wa Kijiji cha Mnero ngongo kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment