Takwimu
zilizotolewa na wizara ya afya, maendeleo ya jamii jinsia , watoto na
wazee nchini zinaonyesha kuwa mkoa wa Dar es salaam na Dodoma inaongoza
kwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja
Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam waziri wa wizara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu alisema
kutokana na hali hiyo wizara imepiga marufuku matumizi ya vilainishi
vinavyotumiwa na baadhi ya makundi yanayo jihusisha na vitendo hivyo.
Mhe. Ummy Mwalimu alisisitiza
kuwa serikali imeamua kuzuia vilainishi hivyo kwani vimetajwa kuchochea
vitendo hivyo ambavyo nikinyume na sheria na taratibu za nchi
nakuongeza kuwa vitendo hivyo nimiongoni mwa sababu inayochangia
ongezeko la VVU.
Aidha Mhe. Ummy alisema kuwa kwa sasa serikali inajikita kuhakikisha kuwa inajenga wodi za wazai, kununua vifaa tiba, madawa ya kutosha katika hosptali zake na sio ununuzi wa vilainishi hivyo.
0 comments:
Post a Comment