Na: Lilian Lundo-MAELEZO
Mwenyekiti
wa Chama cha UDP John Cheyo amewataka Watanzania kupaza sauti na
kukataa maandamano ya Septemba Mosi mwaka huu ambayo yameandaliwa na
Chama cha Demokrasia (CHADEMA).
Cheyo
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi
wa habari kuhusu msimamo wake juu ya maandamano hayo.
“Watanzania
wenzangu jambo la kuwaacha watoto wetu kwenda kupambana na Polisi si
jambo zuri, wote tupaze sauti zetu na kusema hapana kwa maandamano ya
Septemba Mosi,” alisisitiza Cheyo.
Alisema
kuwa, ziko njia mbalimbali ambazo Chadema wanaweza kuzitumia kutatua
migogoro, kama vile meza ya mazungumzo na kuachana na maandamano ambayo
yanachochea vurugu na hata kutishia amani ya nchi.
Aliongeza
kuwa Jeshi la Polisi linapotoa katazo la maandamano ni lazima utii
uwepo, kwani Polisi wapo kwa mujibu wa Sheria na Katiba. Ikiwa Chama
hicho hakikuridhika na katazo hilo basi wanatakiwa kuonana na Waziri
anayehusika na Jeshi la Polisi.
Akifafanua
zaidi alisema kuwa Rais Magufuli amekuwa akichukua hatua za makusudi za
kutatua matatizo mbalimbali kama vile kupambana na ufisadi, ambapo
viongozi wengi wa Serikali wamesimamishwa kazi au kufukuzwa kutokana na
kujihusisha na masuala ya rushwa.
Mwenyekiti
huyo wa UDP amewataka watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli ili
aweze kutimiza ndoto zake na yale ambayo ameyaahidi kwa ajili ya nchi ya
Tanzania.
Aidha
Cheyo aliwasifu viongozi wa Dini ambao walikaa na Viongozi wa Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kukubali kurudi bungeni bila pingamizi
lolote.
Amewataka
viongozi hao wa dini kuendelea kuzungumzia suala la amani kwa
Watanzania na Viongozi wa kiasa ili kudumisha amani ya nchi.
0 comments:
Post a Comment