Mkutano
wa Wakuu wa nchi na Serikali umemalizika katika mjini Mbabane Swaziland
ambapo Tanzania imeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi muhimu na nyeti ya
Siasa, Ulinzi na USalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-
SADC- (SADC Organ On Politisc, Defence and Security Cooperation) ambapo
nchi ya Angola imeteuliwa kuwa Makamu mwenyekiti wa asasi hiyo.
Jukumu
kubwa la asasi hiyo litakuwa ni kuangalia masuala yote yanahusiana na
Siasa, ulinzi na usalama katika ukanda wa SADC huku changamoto kubwa
ikiwa ni namna ya kutafuta suluhu ya kudumu hususani katika eneo la
Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DRC na Lesotho.
Akizungumzia
mambo muhimu yaliyojiri kwenye Mkutano huo wa 36 wa SADC mjini Mbabane –
Swaziland, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan ambaye alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Magufuli amesema mkutano huo umekuwa wa mafanikio
makubwa na amehimiza ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama katika
kuwaletea wananchi maendeleo.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa nchi wanachama wa SADC kwa
sasa zinatakiwa kuongeza juhudi katika kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi haraka kama hatua ya
kujenga ustawi bora wa wananchi wa kanda hiyo.
Kuhusu
Mpango wa Mfalme wa Swaziland wa III wa kujenga Chuo Kikuu cha SADC
nchini mwake kabla ya mkutano ujao wa SADC hapo mwakani chuo ambacho kwa
kuanzia kitatoa ufadhili wa masomo ya Sayansi,Ugunduzi na Utafiti kwa
wanafunzi wanaotoka kwenye nchi wanachama wa SADC, Makamu wa Rais Samia
Suluhu Hassan amesema mpango huo ni mzuri na utasaidia kutoa wataalamu
wengi hasa wanasayansi katika ukanda wa SADC na serikali ya Tanzania
inaunga mkono mkakati huo.
Kuhusu
Tanzania kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama
kwa nchi za SADC, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dkt Augustine Mahiga amesema Tanzania
itahudumu katika asasi hiyo kwa mwaka MMOJA na anaimani kuwa changamoto
za kisiasa zilizopo katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na
Lesotho zipatiwa ufumbuzi.
Mkutano
wa wakuu wa nchi na serikali wa SADC pia umeiteua nchi ya Swaziland
kuwa mwenyekiti wa SADC na Jamhuri ya Afrika Kusini imeteuliwa kuwa
Makamu Mwenyekiti wa SADC.
Katika
mkutano huo wakuu wa nchi na serikali wametia saini rasimu za maboresho
ya mikataba mbalimbali ya jumuiya hiyo ikiwemo mkataba wa kuboresha
itifaki ya SADC dhidi ya rushwa, maboresho ya itifaki ya ushirikiano wa
siasa, ulinzi na usalama ya SADC na maboresho ya itifaki ya biashara.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Mbabane
Swaziland
1-Sep-16
0 comments:
Post a Comment