Adverts

Showing posts with label Afya. Show all posts
Showing posts with label Afya. Show all posts

Monday, October 3, 2016

Rais MagufuliJP amteua Prof. Lawrence Mujungu Museru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 03 Oktoba, 2016 amemteua Prof. Lawrence Mujungu Museru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Lawrence Mujungu Museru umeanza jana tarehe 02 Oktoba, 2016.

Kabla ya Uteuzi huo Prof. Lawrence Mujungu Museru alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

03 Oktoba, 2016

Tuesday, August 30, 2016

Wanaotafuta baba za watoto wao,kutaja waliofanya mapenzi nao Ujerumani

Wanaotafuta baba za watoto wao,kutaja waliofanya mapenzi nao Ujerumani

Wizara ya sheria Ujerumani inapendekeza sheria mpya ambayo itawalazimisha wanawake wanaoshinikiza kutambua baba ya wanao kutoa taarifa ya wanaume waliofanya mapenzi nao wakati wa kutunga mimba. 

Hatua hii inawalinda wanaume ambao wamekua wakitoa ada ya malezi ya watoto ambao baadaye hugunduliwa ktokuwa wao.

Huenda mwanamume kama huyo akalipwa fidia ya kulea mtoto asiye wake kwa miaka ishirini. 

Waziri wa sheria wa Ujerumani, Heiko Mass amesema wanawake watakubaliwa tu kutotambua wapenzi wao ikiwa itabainika kabisa kwamba wanaume wanaotakiwa kutoa ada ya malezi ni baba halisi ya wanawe.

Hata hivyo sheria hiyo lazima ipitishwe na baraza la mawaziri na bunge kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria. 

Chanzo: BBC Swahili

Tuesday, March 8, 2016

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Ataka Makahaba wanaojiuza Pamoja na Wanaume Wanaowanunua Wakamatwe

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza kuiunga mkono Polisi nchini katika operesheni ya kukamata wateja wa makahaba kuhakikisha biashara hiyo inakoma nchini.

Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu alisema takwimu zinaonesha wanawake ndio waathirika wakubwa wa ugonjwa wa Ukimwi, ambapo kati ya Watanzania 100 wanaopimwa, sita ni wanawake na wanaume ni wanne pekee.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Dar es Salaam jana, Ummy alisema si haki kuwakamata wanawake wanaojiuza na kuwaacha wateja wao ambao ni wanaume.

“Ninalipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua hiyo kwa sababu imeonesha kutoegemea upande mmoja kwa kuwakamata wanawake makahaba. Wote wanaojiuza na wanaonunua huduma hiyo ni wakosaji wanaostahili kuchukuliwa hatua za kisheria.Tunaungana na Polisi kushiriki operesheni hiyo,” alisema.

Alieleza kuwa, biashara ya ukahaba inayofanywa na wanawake isingekuwepo endapo wateja wasingekuwepo, hivyo, wateja wanastahili kukamatwa pia kwa sababu ndio wanaoichochea.

Ummy alisema familia nyingi zina misukosuko na wanawake wengi wamekuwa wakiteseka na wengine kuambukizwa magonjwa na waume zao wanaoshiriki biashara hiyo.

Katika hatua nyingine, alisema sasa wanataka kuona idadi ya wanaume wateja wa biashara hiyo inatajwa sambamba na ya wanawake wanaokamatwa nao ili ndugu na wake zao wafahamu kuhusu tabia yao hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki, alisema hatua ya kukamata wateja na wauza miili imetokana na makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Dar es Salaam.

Tuesday, March 1, 2016

Wauguzi sita Temeke wasimamishwa Kazi kwa kuuza gloves


Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamis Kigwangalla amewasimamishwa kazi wauguzi sita katika hospitali  ya  Temeke kwa kosa la kuomba rushwa.

Wauguzi waliosimamishwa ni Hadija Salum, Beatrice Temba, Agnes Mwampashe, Elizabeth Mwilawa, Mariam Mohamed na Marion Said, ambao walikuwa zamu katika wodi ya wajawazito wakati wa tukio hilo.

“Nimewasimamisha kazi wauguzi wote waliokuwa zamu jana (juzi) asubuhi, nakuagiza Msajili wa Baraza la Wauguzi uwasimamishe hadi utakapowasafisha kupitia kamati ya msajili,” alisema Dk Kigwangalla.

Mmoja wa wajawazito, Loshan Seif alisema alipowasili juzi asubuhi kwa ajili ya kujifungua, muuguzi mmoja wa zamu alimtaka kulipia Sh5,000 za gloves.

“Siku zote huwa natumia bima lakini jana (juzi) wakaniambia hawatumii, nitoe Sh5,000 za gloves, baadaye niliambiwa natakiwa kuwa na uzi wa mshono, sindano na vingine hivyo kama sina nitoe fedha,” Seif.

Dk Kigwangalla alifanya ziara ya ghafla hospitalini hapo jana saa 9.00 alasiri.

Akizungumza jana alasiri baada ya kufanya ziara ya ghafla Hospitalini hapo na kupata malalamiko hayo kutoka kwa wanawake waliojifungua.

“Mama anaambiwa atoe fedha ya gloves Sh5,000 wakati dukani zinauzwa Sh1,000, nataka liwe fundisho kwa wote wanaotuongezea vifo vya wajawazito kwa tamaa ndogondogo,” alisema Kigwangalla.

Katika ziara hiyo, Dk Kigwangalla alishuhudia ubovu wa vyumba viwili vya upasuaji na kutoa maelekezo kwamba, virekebishwe ndani ya miezi sita.

“Hali ni mbaya ndani ya hizi ‘theater’ zote mbili zifanyiwe ukarabati iwapo itashindikana nitazifunga, lazima ziwe na hadhi yake na nitakuja kukagua,” alisema.