Wizara ya sheria Ujerumani
inapendekeza sheria mpya ambayo itawalazimisha wanawake wanaoshinikiza
kutambua baba ya wanao kutoa taarifa ya wanaume waliofanya mapenzi nao
wakati wa kutunga mimba.
Hatua hii inawalinda wanaume ambao wamekua wakitoa ada ya malezi ya watoto ambao baadaye hugunduliwa ktokuwa wao.
Huenda mwanamume kama huyo akalipwa fidia ya kulea mtoto asiye wake kwa miaka ishirini.
Waziri
wa sheria wa Ujerumani, Heiko Mass amesema wanawake watakubaliwa tu
kutotambua wapenzi wao ikiwa itabainika kabisa kwamba wanaume
wanaotakiwa kutoa ada ya malezi ni baba halisi ya wanawe.
Hata hivyo sheria hiyo lazima ipitishwe na baraza la mawaziri na bunge kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment