Adverts

Showing posts with label Bongo Flava. Show all posts
Showing posts with label Bongo Flava. Show all posts

Friday, August 26, 2016

Wasanii Wapenda Amani Waungana Kupinga Maandamano UKUTA Ya Chadema


WASANII mbalimbali wanaopenda amani wameungana kwa pamoja kupinga maandamano ya UKUTA yanayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi, mwaka huu.
 
Akizungumza jana mbele ya Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Wasanii hao wapenda amani, Steve Nyerere alisema hamna haja ya maandamano bali tunahaja ya kufanya kazi hususan kwa vijana.
 
"Vijana ndio muhimili mkubwa kulinda amani ya nchi,tusiwaze maandamano bali tuwaze je Akinamama na Watoto wanapata huduma hospitali"alihoji Steve Nyerere.
 
Kwa Upande wa Makamu Mwenyekiti wa Wasanii hao, Asha Baraka alisema wameamua kupaza sauti zao kwa niaba ya Wasanii wote wanaopenda amani.
 
Alisema Tanzania ni nchi ya Amani sio nchi ya vita hivyo wanapofanya shughuli za UKUTA shughuli zote za kijamii zitasimama.
 
Hatahivyo aliomba Septemba 1,  UKUTA wasimamishe maandamano hayo, pia watafute njia muafaka ya kuweza kuongea Vyama kwa Vyama na wakapata muafaka ili nchi iweze kwenda mbele.

Sunday, March 20, 2016

Msanii Chid Benz Anatia HURUMA....Msaada wa Haraka Unahitajika Ili Kumuokoa

Hivi ndivyo Chidi Benz anavyoonekana  kwa sasa.
 
Katika mitandao ya kijamii Jumamosi iliyopita kulisambaa picha za rapa Chidi Benz ambazo zinamuonyesha jinsi alivyokonda na kupoteza ule mwili wake wa kuvutia aliokuwa nao zamani.

Mkali huyo wa wimbo Dar es Salaam Stand Up, anakubalika na vijana wengi kutokana na uwezo wake wa kuandika pamoja na kuchana. Lakini miaka ya hivi karibuni alianza kubadilika baada ya kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Oktoba 24 mwaka 2014, Chidi alikamatwa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere wakati akielekea jijini Mbeya kwa ajili ya show. Lakini kesi hiyo ilimalizika miezi michache baadaye baada ya kuamriwa na mahakama kulipa faini.

Tukio hilo liliwafanya wasanii mbalimbali kuzungumzia hali hiyo huku wakimshauri kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya. Ray C ambaye ni mmoja kati ya waathirika janga hilo ambaye kwa sasa yupo kwenye tiba ya methadone, aliamua kumshauri Chid Benz.

“Pole kaka yangu Chidi Benz. Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo bado haujalitafutia jibu la kutatua tatizo lako. Mimi ni dada yako natumeshafanya kazi pamoja, tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani,” aliandika Ray C kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo Chidi Benz aliendelea na harakati zake huku akijinadi katika vyombo vya bahari kwamba tayari ameshaachana na matumizi ya madawa ya kulevya. Lakini watu wake wa karibu pamoja na marafiki zake walikuwa wanadai kwamba bado hajaacha.

Lakini Jumamosi hii akiwa katika kipindi cha Da Weekend Chart Show cha Clouds TV, Chidi amelionekana amechoka zaidi huku akiowamba wadau mbalimbali kumsaidia.

“Matatizo yangu na stress zangu ambazo niko nazo zinanisababishia mwili wangu unapungua kwasababu siko okay, siko poa, siko sawa yaani,” alisema.

Mmoja kati ya wasanii wakongwe wa muziki wa Hip Hop, Afande Selle, alionyesha kusikitishwa na jinsi madawa ya kulevya yanavyomaliza nguvu kazi ya taifa.

 “Yanapita kwa njia gani madawa ya kulevya hapa nchini? Anayasambaza nani mitaaani kote mitaani? Madawa ya kulevya hayaleti maendeleoooo,madawa ya kulevya yanaua masela leooooo,” alisema Afande Selle.

Pia wadau mbalimbali wamewataka watu pamoja na wasanii wenzake kumsaidia huku Arnold Kayanda, mtangazaji wa BBC Swahili akisema amelipokea kwa masikitiko suala hilo.

“Kama picha hii ni rafiki yangu Chidi Benz kama nilivyotaarifiwa, kwa hisani yenu wote naomba kila mtu kwa nafasi yake amsaidie. Mimi niko mbali lakini nikirudi nitakutana naye,” alisema.

Licha ya wadau mbalimbali kutaka asaidiwe lakini bado tunaona hakuna msaada wa haraka ambao mpaka sasa umechukuliwa ili kumuokoa Chidi Benz. 

Serikali ya Magufuli ni sikivu sana, bila shaka kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inayoongozwa na Waziri kijana mpenda sanaa, Nape Moses Nnauye ataliangalia suala hili.

Wednesday, February 24, 2016

Wasanii Waidai Mamilioni Ya Pesa IKULU....Deni hilo Liliachwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete


Ikulu imeahidi kufanyia kazi madai ya Chama cha Wasanii Wachoraji Tanzania (Chawata), ambayo waliyawasilisha jana, kikilalamikia ofisi hiyo katika awamu ya nne iliyokuwa chini ya Rais Jakaya Kikwete, kuwacheleweshea malipo yao ya Sh. milioni 53.6.

Kwa mujibu wa taarifa ya Chawata kwa vyombo vya habari jana, fedha hizo zimetokana na kazi za sanaa ambazo zilichukuliwa na serikali ya awamu ya nne kutoka kwa wafanyabiashara wa eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam na kupelekwa Ikulu.

Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, alithibitisha kuwapo na madai hayo na kusema kuwa yatafanyiwa kazi ndani ya wiki moja kuanzia jana.

“Ni kweli Ikulu inadaiwa, lakini ni deni la awamu ya nne, kwa hiyo tumewaomba kuwakamilishia madai yao ndani ya wiki moja, baada ya kufanya uhakiki ili kujiridhisha,” alisema Msigwa.

Awali, Katibu wa Chawata, Cuthbert Semgoja alisema waliahidiwa kulipwa fedha hizo kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana lakini hadi sasa hawajalipwa.

"Tuliuza kazi zetu Ikulu kwa makubaliano ya kulipwa baadaye tangu Agosti mwaka jana, hadi leo hii (jana) bado hatujaweza kupatiwa pesa zetu," alisema na kuongeza:

“Mchakato wa kazi zetu ulianza mwishoni mwa mwezi wa nane kwa kamati husika, kupitia katika maeneo ya wasanii, ili kuweza kufanya chaguzi ya sanaa wanazohitaji. Walijiridhisha kwa kuchukua baadhi ya sanaa kutoka kwa wanakikundi kwa ahadi ya kufanya malipo mara moja kabla ya uchaguzi mkuu lakini hadi sasa bado malipo hayo,” alisema Semgoja.

Alisema baada ya chama kuona muda wa malipo unakwisha, walichukua jukumu la kupiga simu kwa mhusika ambaye walikuwa wakifanya naye biashara hiyo kwa niaba ya Ikulu, lakini jibu lake lilikuwa `malipo yenu yanaandaliwa.'

“Baada ya mwezi mmoja kufanya biashara hiyo, tulianza kumpigia simu mtu mmoja ambaye ndiye alikuwa anahusika na sisi tangu mwanzo wa biashara yetu hadi mwisho, lakini majibu tunayopewa ni kusubiri tu, tumechoka sasa,” alisema.

Alisema mawasiliano waliyokuwa wanafanya na mtu kutoka Ikulu ambaye alijitambulisha (jina tunalo), ndiye aliyekuwa akiwapa majibu hayo kuhusu madai yao.

Aliongeza kuwa kulingana na ahadi waliyopewa kulipwa kabla ya uchaguzi mkuu na mlolongo wa ahadi zinazojirudia, walianza kufanya mawasiliano wao kwa wao ili  kufahamu nini kinachoendelea kuhusu malipo yao na kugundua kuwa kuna tatizo.

“Ilifika hatua simu zetu hazipokelewi, kila tunapopiga mhusika hapokei simu zetu, ndipo hapo tulipohisi kuna mchezo unaendelea kati ya mtu huyo na chama chetu,” alisema.

Ray C Alia na Ugumu wa Maisha.....Aeleza mtindo anaotumia kupanda daladala Ili Kukwepa Aibu


Ray C ameweka wazi kuwa yuko taabani kiuchumi, hali inayompelekea kukosa hata pesa ya usafiri wa kwenda hospitali kupata dozi ya tiba ya maradhi yanayomkabili kutokana na kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Akiongea na Planet Bongo ya EATV hivi karibuni, Ray C alieleza kilio chake akidai kuwa sio tu kwamba amekosa pesa ya kuendelea kusapoti muziki wake baada ya aliyeahidi kumsaidia kumkimbia, bali inamlazimu kupanda daladala akiwa ndani ya vazi la ‘ninja’ kutokana na kushindwa gharama za usafiri.

“Jamani kiukweli haya maisha ya wasanii nyie acheni tu, yaani inabidi tumuombe tu mungu, mtu akikuona msanii kwenye daladala nani atanunua albamu yako, nani atakuja kwenye show yako, lakini mama ananiambia vaa ninja mwanangu nenda kapate tiba.  Kwa sababu kila siku kukodi taxi ni gharama sana, kutoa elfu 25,000 kutoka Bunju mpaka hospitali kila siku ni nyingi sana," alieleza.

“Sometimes namwambia mama inabidi tutoke mapema saa 11 hivi nivae ninja twende kwanza kanisani then naweza nikachukua hata bajaji kwenda hospitali. Haya ni maisha sio kitu cha kucheka ni lazima nifanye hivyo ili niweze kumaliza dozi,” aliongeza.

Ray C alieleza kusikitishwa na namna ambavyo baadhi ya magazeti yanamuandika na kumchafulia jina kwa kile alichodai ni habari za kutungwa kuwa amerudia dawa za kulevya, badala ya kuandika habari njema zinazomhusu.

Mwimbaji huyo ambaye album yake imekwama studio, aliwaomba wadau na wananchi kwa ujumla kumsaidia hata kwa kumchangia kiasi kidogokidogo cha fedha ili aweze kumudu gharama za maisha na hata kurejea jukwaani.