Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka
jeshi la polisi nchini kurejesha kitengo cha ulinzi bandarini na pia
eneo ambalo linafungwa mita za mafuta.
Taarifa
ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imesema Rais Magufuli
ametaka jeshi la polisi nchini kurejesha ulinzi kama ilivyokuwa nyakati
za nyuma kabla mamlaka ya bandari haijaamua kubandilisha mfumo wa kuweka
walinzi wake.
Balozi
Ombeni Sefue ameongeza kuwa katika eneo ambalo linafungwa mita za
mafuta (Flowmeters), ambalo waziri mkuu alitembelea na kumsimamisha
mkurugenzi wa wakala wa vipimo sasa ni lazima lilindwe na jeshi la
polisi.
0 comments:
Post a Comment