Maafisa wa Marekani wamethibitisha kuwa ni ndege za Marekani zilizofanya mashambulio huko Libya wakiwalenga wanamgambo wa IS.
Hata
hivyo shambulio hilo la karibu na mji wa Sabratha,lililonuiwa kumlenga
hasa mpiganaji mmoja wa Tunisia limeripotiwa kuwauwa watu 30.
Mpiganaji
huyo wa Tunisia anasemekana ndiye aliyefanya shambulio la mwaka jana
katika kumbukumbu za Bardo na hoteli ya ufuoni mwa bahari ya Sousse huko
Tunisia ambako watu zaidi ya 10 waliuawa.
Mashambulio hayo yalilenga kambi moja ya wapiganaji wa Islamic State
na kumuua kiongozi mmoja mwenye itikadi kali ,maafisa wa Marekani
wamesema.
Noureddine Chouchane anahusishwa na mashambulio mawili
nchini Tunisia mwaka uliopita ,ikiwemo shambulio lililowaua raia 30 wa
Uingereza.
Kundi la IS limekuwa likifanya oparesheni zake nchini
Libya kwa kipindi cha mwaka mmoja na Marekani inakadiria kwamba lina
hadi wapiganaji 6,000 nchini humo.
Libya inasalia katika machafuko ya wenyewe kwa wenyewe miaka minne baada
ya kupinduliwa kwa aliyekuwa kiongozi wake Muammar Gaddafi,na
inapiganiwa na makundi tofauti ikiwemo kundi la IS.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment