Walalmishi wawili wameshindwa katika
jaribio lao la kuishinikiza mahakama ya kikatiba nchini Ujerumani
kuangazia madai yao dhidi ya sheria inayopiga marufuku kujamiana na
wanyama.
Watu hao ambao majina yao hayakutajwa wanasema kwamba wana uchu na wanyama.
Walitaka kuishinikiza mahakama hiyo iliopo Karlsruhe kufikiria iwapo sheria hiyo ni kinyume na katiba.
Hatahivyo mahakama hiyo ilitupilia mbali madai yao ikisema kuwa ni haki kwa sheria hiyo kuendelea kufuatwa.
Mahakama
ilisema kuwa kuwalinda wanyama dhidi ya unyanyasaji wa kingono ni
jukumu la sheria ,ambayo haikubadilishwa kufuatia uamuzi wa mahakama
hiyo.
Sheria za kuwalinda wanyama nchini Ujerumani zimeweka faini
ya $27,700 kwa wale watakaowalazimisha wanyama kushiriki katika tabia
mbaya.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment