Waziri wa nchi
ofisi ya rais TAMISEMI, utumishi na utawala bora, George Simbachawene wa
kwanza kushoto akiwaambia jambo mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist
Ndikilo wa katikati na wa kulia mganga mkuu hospital ya Rufaa ya Tumbi
dk. Peter Datan wakati alipotembelea shirika la elimu Kibaha juzi.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
***
Waziri
wa nchi ofisi ya rais TAMISEMI, utumishi na utawala bora, George
Simbachawene amesema ataunda tume ya watu wachache kutoka wizara hiyo
haraka iwezekanavyo ili kuchunguza idara na vitengo vyote katika shirika
la elimu Kibaha (KEC) ndani ya wiki mbili.
Amesema
amefikia hatua hiyo baada ya kubaini tatizo kubwa la uongozi hivyo ipo
haja ya kuchunguza hali iliyopo kuanzia juu hadi chini.
Aidha
Simbachawene alisema tume hiyo itakuwa na kazi ya kupita kila idara na
kitengo kuchunguza mambo atakayoyaelekeza kwa siku 14 kisha mwezi march
mwaka huu atarejea kufanya ziara na kuzungumza na watumishi.
Alielezea
kuwa kuna kila sababu ya kutafakari muundo mzima wa shirika na kuweka
mikakati, sheria na mipango ya kisasa na kuondokana na ile iliyopitwa na
wakati.
Aliyasema
hayo juzi katika ziara yake ya kikazi ya siku moja aliyoifanya shirika
la elimu Kibaha ambapo alipata fursa ya kutembelea maeneo ya uwekezaji
na shirika kijumla.
Simbachawene
alisema katika shirika hilo kuna wachache wanaonufaika na kuneemeka kwa
kula hadi wamevimbiwa huku wengine wakiwa wanadidimizwa kimaslahi na
kukosa haki zao za msingi.
Alimtaka
mwenyekiti wa bodi mpya ya shirika hilo Patrick Makungu na viongozi
wengine katika bodi hiyo, kuwa na mawazo mapya ya kuendesha shirika
badala ya kufanya kazi kwa mazoea ili kurudisha maendeleo yaliyokuwepo
miaka ya nyuma.
Alisema
shirika la elimu Kibaha lina miradi mingi, ardhi kubwa na uwekezaji
mkubwa hivyo waitumie kujiongezea kipato kwa maslahi ya Taifa na vizazi
vijavyo.
Simbachawene alieleza KEC inayumba na kuondoa taswira ya maendeleo na uchumi wake wakati ina vitega uchumi na ardhi kubwa.
“Serikali
ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli ipo kwa ajili ya kuinua uchumi
wa nchi na haitokuwa tayari kuona mashirika ya aina hii yanashushwa
hadhi yake na watu wachache na kuwanyima haki watumishi uhuru wa
kutembea kiajira na haki zao za msingi “
” Ipo haja ya kuchunguzana na kufanya maamuzi makini kwa kufuata misingi, sheria, kanuni na haki za kiutumishi”alisema Simbachawene.
Hata
hivyo alisema uwekezaji wa kampuni ya organia kutoka Egypt iliyowekeza
kwenye shirika hilo ni mzuri na wenye tija lakini unaonekana haufuata
taratibu na kusababisha maswali kutoka kwa watumishi.
Awali
mkurugenzi wa shirika la elimu Kibaha Dk. cyprian Mpemba alisema
shirika linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupokea wagonjwa
wengi 400 hadi 450 kwa siku na madawa.
Dk.
Mpemba alitaka serikali kufikisha fedha kwa wakati kwani ni muda mrefu
sasa fedha wanazoahidiwa wanatumiwa pungufu tofauti na kiwango
wanachoomba hivyo kushindwa kukidhi mahitaji.
Nae
mganga mkuu wa hospital ya Rufaa ya Tumbi, dk. Peter Datan alisema
kitengo cha maafa hususan ajali (Trauma center) kinakabiliwa na ukosefu
wa fedha kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
Katika
hatua nyingine waziri huyo alipokea kero mbalimbali kutoka kwa
watumishi wa shirika hilo ikiwa ni sanjali na wastaafu shirikani hapo
kukosa stahiki zao.
Kero
nyingine ni kuondolewa mradi wa kuku ulikuwa ukiingiza bil. 1 na
kuingizwa mradi wa mkataba wa Organia ambao hawauelewi maslahi yake,
upungufu wa nyuzi, madawa, fedha za allowance na walimu kutopandishwa
madaraja kwa miaka sita sasa.
Simbachawene
alipokea kero hizo na kuahidi kuzifanyia kazi ambapo kwa upande
mwingine aliitaka mganga mkuu dk. Datan kukumbushia fedha walizoahidiwa
serikalini ili ombi lao lishughulikiwe haraka.
0 comments:
Post a Comment