Mwandishi wa Habari wa Radio Deutsche Welle(DW-Swahili), Salma Said jana alikamatwa na watu wasiojulikana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Unguja, alipokuwa akisafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia afya yake.
Akizungumzia
tukio hilo jana, mume wa Salma, Ali Salim Khamis ambaye pia ni Mbunge
wa Mwanakwerekwe (CUF), alisema alipata ujumbe wa maandishi kutoka kwa
mkewe kwamba amekamatwa.
Khamis
alisema alipokwenda uwanja wa ndege aliambiwa na mkuu wa polisi wa
uwanjani hapo kwamba hana taarifa za tukio hilo jibu ambalo alilipata
pia kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mjini Magharibi.
Alisema aliamua kwenda kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambako pia aliambiwa hawana taarifa za kukamatwa kwa Salma. “Hadi sasa sijui mke wangu yuko wapi bado naendelea kumtafuta.”
Khamis
alisema Salma alikuwa tayari amepitia taratibu zote na alikuwa
akisubiri kuingia ndani ya ndege ambayo haikutajwa, lakini alisema ndege
hiyo iliyokuwa iondoke saa 8.05 mchana ilizuiwa na watu hao wanaodaiwa
kuwa ni askari hadi saa tisa kasoro, walipoiruhusu lakini ikidaiwa kuwa
waliondoka na Salma kwenda kusikojulikana.
0 comments:
Post a Comment