Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, amesema Benki ya Standard inapaswa kuchunguzwa kwa rushwa kuhusu suala la hati fungani ya Dola za Marekani milioni 600.
Amesema
kwa sasa deni la Taifa limepanda na kufikia dola bilioni 15 sawa na Sh
trilioni 30, ambapo kutokana na ukubwa wa deni hilo, Tanzania hulipa
huduma ya deni la Taifa takribani Sh trilioni 2.2 kila mwaka.
Alisema licha ya hali hiyo bajeti ya kuhudumia deni la Taifa ni kubwa zaidi kuliko bajeti ya wizara yoyote nchini.
Alisema
kutokana na suala hilo katika madeni hayo yapo ambayo yamepatikana kwa
rushwa na mengine yamechukuliwa kwa matumizi ya anasa.
“Kitaalamu
madeni haya yanaitwa ‘Odious debts’. Moja ya Deni la hovyo ni la dola
za Marekani milioni 600 ambalo Tanzania ilikopa kutoka Benki ya Standard
ya Uingereza kupitia hati fungani.
“Taasisi
ya SFO ya Uingereza inayoshughulika na rushwa kubwa imeonyesha kuwa
mkopo huu ulipatikana kwa rushwa. Taasisi ya Corruption Watch ya
Uingereza imeonyesha kuwa Tanzania imepata hasara ya takribani dola
milioni 80 sawa na bilioni 160 kwa kuchukua mkopo huu.
“…
hata hivyo uchunguzi wa SFO haukuhusisha maofisa wa juu wa Standard
Benki makao makuu na hivyo kufunika kombe mwanaharamu apite.
“Iwapo
uchunguzi ungegundua kuwa Standard Benki walihusika moja kwa moja na
hongo hii, Tanzania ingefutiwa deni lote na kuokoa fedha nyingi sana
ambazo zingewekezwa kwenye sekta za elimu, afya na maji,” alisema Zitto.
Mbunge
huyo wa Kigoma Mjini, alisema wanaitaka Benki ya Standard ya Uingereza
ichunguzwe upya na SFO kuhusu tuhuma za rushwa ili kupata biashara
Tanzania ya hati fungani pamoja na kujua ukweli wa kile alichodai
ufisadi huo.
Kutokana
na hali hiyo alisema wameandaa maombi kwa kuitaka FSO ya Uingereza
ifungue upya uchunguzi kwa kuzingatia ushahidi mpya kuwa mabosi wa Benki
ya Standard ya Uingereza walihusika na mipango ya kutoa hongo ili
kupata biashara Tanzania.
Alisema
ikibainika mabosi hao walishiriki maana yake Tanzania itafutiwa deni
lote kwa sababu benki hiyo itawajibika kurudisha fedha za watu kwani
Hati fungani itaonekana ni batili.
Zitto
alisema hivi sasa Tanzania inaanza kulipa deni hilo kuanzia Aprili,
mwaka huu na kama wasipozuia tunazuia kwa maombi haya kwa FSO.
Alisema
iwapo deni hilo litalipwa juhudi za Rais Dk. John Magufuli, kupata
mapato zitaathiriwa na sekta nyeti kama elimu, afya na maji zitakosa
bajeti ya kutosha.
Alisema
kutokana na hali hiyo aliwaomba Watanzania kote duniani kuitaka SFO
ifungue uchunguzi kwa kuzingatia ushahidi mpya dhidi ya Benki ya
Standard ambayo sasa inaitwa ICBC plc
0 comments:
Post a Comment