Picha ya maktaba
Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, wilayani Kilombero jana lilimkamata mbunge
wa jimbo la Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali kwa madai ya kutaka kuingia
katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kuapisha na kuchagua mwenyekiti
na makamu wake wakati si mpigakura.
Lijualikali alikamatwa nje
ya ukumbi wa halmashauri na polisi na kuswekwa rumande katika Kituo
Kikuu cha Polisi Wilaya ya Kilombero saa 3.48 asubuhi wakati akiingia
kwenye ukumbi huo kama mmoja wa mashuhuda.
Mwenyekiti wa Chadema
Wilaya ya Kilombero, Shabaan Mikongolo alisema mbunge huyo hakutendewa
haki na polisi kwa kuwa alifika eneo hilo kushuhudia matukio ya
kuapishwa kwa madiwani.
“Ni kama kuna maelekezo yalitolewa kwa
polisi kuwazuia wabunge, Lijualikali na Devotha Minja (Viti Maalumu –
Chadema) na mwakilishi wa Katibu Mkuu Chadema kutoingia ukumbini lakini
viongozi wengine wa Serikali ngazi ya mkoa na wilaya waliruhusiwa." Alisema Mikongolo
Pia,
polisi walizuia waandishi wa habari na kutaka
kuwanyang’anya kamera zao kwa sababu ambazo hazikuwekwa bayana.
Katika
uchaguzi huo, Diwani wa Sanje (CCM), David Ligazo alichaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilombero kwa kura 19 dhidi ya Godfrey
Lwena ( CHADEMA) aliyepata kura 18
0 comments:
Post a Comment