Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
amewataka wanachama wenzake wa Chama Cha Mapinduzi CCM,kuiacha
Demokrasia ichukue mkondo wake katika suala la uchaguzi wa meya wa jiji la Dar es Salaam kwa kuwa asiye kubali kushindwa si mshindani.
" Suala la umeya Dar es salaam liachwe demokrasia ichukue mkondo wake.
Na niwaombe wana CCM wenzangu tusilazimishe mambo, tukubali kushinda
lakini pia tukubali kushindwa. Mahali tunapostahili kushinda kama
tumeshinda basi tushinde kweli. Lakini mahali tunaposhindwa basi
tukubali kushindwa na hiyo ndiyo Demokrasia ya kweli. Akishinda mwana
CCM ni sawa, akishinda wa CHADEMA ni sawa....sisi tunachotaka ni
maendeleo ya watu wa Dar es salaam"- Alisema Rais Magufuli
0 comments:
Post a Comment