Mtandao
wa Wanawake wa Katiba na Uchaguzi, umemuomba Rais John Magufuli
kusimamia kikamilifu utekelezwaji wa mikataba iliyosainiwa na Tanzania
katika usawa wa kijinsia ili kupunguza pengo lililopo kuelekea usawa wa
50/50 katika nafasi za uongozi.
Maombi
hayo yamekuja kufuatia uteuzi wa wakuu wa mikoa uliofanywa mwishoni mwa
wiki iliyopita na wanawake waliopenya kuwa ni watano kati ya wateule
26, ikiwa ni sawa na asilimia 20.
Taarifa
hiyo iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia (TGNP),
Gloria Shechambo ilielezea kuwapo kwa dalili za kuwakandamiza wanawake
kutokana na idadi ndogo ya wanaoteuliwa kushika uongozi katika ngazi za
uamuzi.
Mkurugenzi
wa TGNP, Lilian Liundi aliwahi kusema kuna makatibu wakuu wa wizara
mbalimbali na manaibu wao 50, huku wanaume wakiwa 40 sawa na asilimia
80.
0 comments:
Post a Comment